MATANGAZO YA TAREHE 29.10.2023
DOMINIKA YA 30 YA MWAKA “A”.
Soma ZaidiNeema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Asante kwa kutembelea tovuti yetu, karibu sana kusoma kwenye tovuti ya Kanisa Katoliki, Parokia ya Utatu Mtakatifu - Changanyikeni. Jimbo kuu la Dar es Salaam
Ninayo furaha ya pekee kwa niaba ya wanaparokia wote wa Parokia ya Utatu Mtakatifu - Changanyikeni, kukualika ndugu msomaji ushiriki na wanaparokia wa parokia yetu kuieneza Injili ya Yesu Kristu kupitia tovuti hii.
Parokia yetu ya Utatu Mtakatifu - Changanyikeni ina asili yake iliyojengwa katika misingi ya Umoja, Upendo na Ushirikiano ulioanzia mwaka 1995.
“Kuwa Parokia Imara na Mahiri katika masuala ya Kiroho, Kijamii, na Kiuchumi ambayo yatasimikwa juu ya misingi ya Umoja na Upendo wa Kimungu”.
“Parokia kujizatiti kikamilifu katika majukumu ya uinjilishaji ili kuwaimarisha waamini Kiroho, Kijamii na Kiuchumi kwa njia ya utoaji wa huduma bora kwa watu wote na kwa usawa”.
Mawasiliano thabiti nyakati zote
Historia ya parokia ya Utatu Mtakatifu ina asili yake iliyojengwa katika misingi ya Umoja, Upendo na Ushirikiano ulioanzia mwaka 1995.
Wazo la ujenzi wake liliwahusisha mlezi wa chaplaincy ya Chuo KikuuPadre Severine Msemwa, wakatoliki waishio Changanyikeni na Parokia ya Mtakatifu Paulo Msewe. Kwa pamoja walikubaliana huduma za kiroho kutolewa sehemu ya Changanyikeni, hasa kutokana na changamoto kubwa ya kuvuka mto wakati wa masika kwenda Msewe na pia ukweli kwamba huduma za kiroho za chaplaincy ya Chuo Kikuu ilikuwa mahususi kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo Kikuu hali ambayo haikukidhi mahitaji ya walei kikamilifu. Waamini wa Changanyikeni waliunda uongozi mdogo wa kuongoza kikundi chao cha sala, mwenyekiti akiwa Richard Silo, KatibuLaura mapunda, na Katibu msaidizi akiwa Fortunatus Mkawe.
Parokia ya Mt. Paulo Msewe na Chaplaincy ya Chuo Kikuu waliendelea kwa pamoja kuwahudumia waumini wa changanyikeni, kusimamia na kupitisha mpango wa kujenga kigango cha Changanyikeni kati ya mwaka 1996 mpaka 2002. Mfano masuala yote ya kiutawala ya wanachanganyikeni yalishughulikiwa na parokia ya Mt. Paulo Msewe na masuala ya kiroho yalishughulikiwa na Parokia ya Chuo Kikuu. Aidha wakati wote mwakilishi wa waumini wa Changanyikeni ndugu Richard Sillo alikuwa akishiriki mikutano yote katika parokia zote mbili. Kila jambo lilifanyika katika hali ya ushirikiano (Waumini wa Changanyikeni + Chuo Kikuu + Ubungo Msewe).