Vyama Vya Kitume

Vyama Vya Kitume

Parokia ya Utatu Mtakatifu, Changanyikeni ni vyama vya kitume vifuatavyo, WAWATA, VIWAWA, UKWAKATA, MOYO MTAKATIFU WA YESU, MT RITA, KARISMATIKI, SHIRIKA LA WAZEE NA WASTAAFU, LEGIO MARIA,MT. VINCENT WA PAULO, na MT ANNA.

WAWATA ni Jumuiya wa Wanawake wa Katoliki wa Tanzania. Jumuiya hii ilianzishwa mnamo mwaka 1972, kwa kuzingatia misingi ya katiba ya muungano wa Jumuiya za Wanawake Wakatoliki Duniani WUCWO {World Union of Catholic Women Organisation }iliyosajiliwa chini ya sheria ya Uswiss, 1910. Washiriki wa jumuiya ya WAWATA ni kila mwanamke na msichana mbatizwa kuanzia  miaka 14 ni mwanachama wa jumuiya hii.WAWATA Parokia ya Utatu Mtakatifu ni chama cha Kitume kinachofanya kazi zake chini ya mwongozo wa katiba ya Halmashauri Walei Tanzania na Katiba ya WAWATA Tanzania.

DIRA: Taswira ya Jumuiya ya Wanawake wa Katoliki Tanzania (WAWATA) , ni kuona kila Mwanamke Mkatoliki wa Tanzania anaelewa nafasi yake na wajibu wake wa kikristu kuanzia ngazi ya Familia, Jumuiya, Kanisa, Jamii na Taifa.

DHAMIRA: Kwa Upendo wa Kristo! Tutumikie na Kuwajibika.

              MALENGO YA JUMUIYA YA WANAWAKE WA KATOLIKI (WAWATA):

  1. Kuwaunganisha Wanawake Wakatoliki nchini Tanzania, katika juhudi zao zinazohusu kama wakristo, wanawake, na raia wakiwa katika vikundi mbalimbali ambavyo hasa lengo lao ni kulistawisha kanisa na jamii.
  2. Kuwahamasisha wanawake hao, ili waweze kushirikiana na waamini wote katika kujenga familia bora za kikristo popote nchini.
  • Kuwatia moyo Wanawake Wakatoliki  katika kujiendeleza na kutambua hadhi yao, kama wanawake katika kanisa ili waweze kutimiza wajibu wao kikamilifu kama waumuini wote wanavyotakiwa.
  1. Kuwawezesha Wanawake Wakatoliki wote kushiriki katika shughuli zote za Halmashauri Walei Tanzania kama wana Halmashauri kamili na pia katika vyama vingine vya kitume kwa kadri ya uwezo, tokea Jumuiya ndogo ndogo, vigango, Parokiani, Jimboni hadi Kitaifa na Kimataifa.
  2. Kuwaelimisha na kuwahimiza WAWATA kwa kila njia ili wawe na uwezo wa kushiriki kikamilifu pamoja na wanawake wote wa Tanzania katika shughuli zote za maendeleo ya Wanawake nay a nchi kwa ujumla, kiuchumi,kisiasa, pia kujiunga katika mashirika na vyama mbalimbali vya wanawake nchini visivyopingana na maadili ya Kanisa Katoliki.
  3. Kushiriki na Wanawake Wakatoliki wa Dunia kama kiungo cha WUCWO ili kujenga dunia yenye Usawa, Haki na Amani.

Kuwawezesha Wanawake Wakatoliki Tanzania, kuwakilishwa katika vikao mbalimbali vya WAWATA, Kanisa, Halmashauri Walei kwa ujumla katika maendeleo mbalimbali

UONGOZI

S/N

WADHIFA

JINA

KANDA

SIMU

1

MWENYEKITI

ROSE KISUSI

MT. BERNADETHA

 

2

MAKAMU MWENYEKITI

FRANSISCA KAYUMBO

MT. ANYESI

 

3

KATIBU

MARY KAYOMBO

MT. ANNA

0653 – 795757

4

KATIBU MSAIDIZI

BRENDA MAKUBI

MT. ANDREA KAGWA

0713 – 435224

5

MWEKA HAZINA

FLORENCE KILASARA

MT. VERONIKA

0754 – 294333

Ni Chana cha kitume cha vijana wakatoliki wafanyakazi ambao tunatumwa na Kanisa ili kueneza habari njema Kamba Yesu Kristu ndie Njia ya ukweli na uzima kwa vijana wote katika Maisha yetu ya kila siku.
Chama hiki kinatuunganisha vijana na kuwasaidia vijana waone hali zao, kuamua juu yake katika mwanga wa injili na kutuongoza tufanye Matendo ya kubadilisha Hali zeta na kutengeneza ziwe nzuri zaidi kwa njia ya Tafakari ya maisha.
DIRA YA VIWAWA
Kumwona Kijana Mkatoliki Mfanyakazi anayejimudu katika maisha yake ya Kimwili na Kiroho kwa kutumia njia ya Tafakari ya Maisha.
MALENGO YA VIWAWA
Kuwawezesha Vijana kutambua wajibu wao katika kujielimisha na kujitegemea katika maisha Yao.
Kustawisha na kusaidia Kansa kwa kushiriki katika Kari za Kansa, kuhusu maendeleo ya kiroho,kimwili, kiakili na kijamii.
Kutangaza habari za Kansa na kujaribu kwa kila Hali kuleta uhusiano mwema Bain’s ya Yama ya kitume, madhehebu mbalimbali na dini nyingine.
Kuwajenga vijana katika mazingira ya kuwa na mwenendo mwema kwa Kanuni ya a Tafakari maisha inayoongozwa na mtindo wa kuona-kuamua na kutenda.
Kuwakumbusha vijana wote kwamba sote tunategemeana kwa kushauriana, kuongozana na kufundishana kimwili na kiroho

UONGOZI

S/N

WADHIFA

JINA

KANDA

SIMU

1

MWENYEKITI

CASTO KOBA

MT. YOHANE PAULO WA PILI.

0659 - 154291

2

MAKAMU MWENYEKITI

TUNU FONGA IDD

MT. VERONIKA

0757 - 783293

3

KATIBU

DAVIDA FELICIAN

MT.

0716 – 300333

4

KATIBU MSAIDIZI

MAXIMILLIAN RWEKIZA

MT. BERNADETHA

0656 - 643582

5

MWEKA HAZINA

AIDAN KAPINGA

 

0686 - 747295

Huu ni Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania ambao una malengo makuu mawili
1. Kutukuzwa kwa Mungu
2. Kutakatifuzwa kwa wanachama wenyewe
Salaam ya UKWAKATA ni: Tumwimbie Bwana-Katika Roho na Kweli (Yoh 4:23)
Utume huu una jukumu kuu la Uinjilishaji kwa njia ya kuimba.
Katika Parokia ya Utatu Mtakatifu-Changanyikeni,UKWAKATA inaundwa na Kwaya Mbili
1. Kwaya ya Utatu Mtakatifu
2. Kwaya ya Mt.Karoli Lwanga
Kwasasa Kuna jumla ya wanachama 70 kutoka Kwaya zote Mbili.
Mlezi wa UKWAKATA ngazi ya Parokia ni Baba Paroko.
Sikukuu ya Ukwakata Kitaifa hufanyika tarehe 22 Novemba ya kila mwaka ambayo ni siku ya Mt.Sesilia.
Mikakati ya UKWAKATA
1. Kuwa na Sherehe ya UKWAKATA kila mwaka yenye lengo la kujenga mahusiano mema kati
ya kwaya zetu na Kupokelewa rasmi kwa wana Ukwakata Wapya.
2. Kuwa na Semina maalum kuhusu uimbaji zitakazo wawezesha wanakwaya kuutambua
vyema wito huu wa uimbaji
3. Kuwa na Hija za kuwaimarisha wana Ukwakata Kiimani
4. Kurekodi Nyimbo na kuzisambaza ndani na nje ya Parokia
5. Kuinjilisha ndani na nje ya Parokia ili kujenga mahusiano mazuri na Parokia nyingine
6. Kuendeleza darasa la muziki ili kuongeza idadi ya wataalam wa muziki Mtakatifu
7. Kuwa Tamasha kubwa la Kwaya kwaajili ya kuboresha uimbaji wetu.

UONGOZI

S/N

WADHIFA

JINA

1

MWENYEKITI

MATHIAS GARIMO

2

MAKAMU MWENYEKITI

AIDAN KAPINGA

3

KATIBU

LAURENT BENEDICTO

4

KATIBU MSAIDIZI

EDITH WAKARA

5

MWEKA HAZINA

WINIFRIDA KAMAMBA

Chama cha Moyo ❤️ Mtakatifu wa Yesu ni ushirika wa waumi wote kuanzia watoto waliokwisha kupokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu yaani komunyo ya kwanza hadi wazee. Ushirika wa Moyo Mtakatifu wa Yesu ndiyo uhai wa kanisa Katoliki. Hapa Parokiani kwetu kilianzishwa mwaka Novemba 2020. mpaka sasa tunao wanachama 29 walio hai.

Lengo kubwa la ushirika huu ni kuungana pamoja katika kumwabudu, kumshukuru, kumtolea sifa na kumwomba Mungu kwa njia ya sala zetu kupitia Moyo huu.

Ratiba ya Ushirika wetu ni kama ifuatavyo:-
1. Kuabudu Ekaristi Takatifu kila alhamisi.
2. Kusali pamoja kila ijumaa ya kwanza ya mwezi kwa heshima ya Moyo Mtakatifu wa Yesu na ijumaa nyingine za wiki.
3. Kusali kwa heshima ya Moyo safi wa mama Bikira Maria kila jumamosi ya kwanza ya mwezi.
3. Kufanya mkutano kila jumapili ya kwanza ya mwezi.
4. Kufanya HIJA, matendo ya Huruma kulingana na kalenda ya Jimbo na ya tawi husika.

Matarajio yetu ni kutaka kila mmoja wetu katika Parokia na mahali popote wamjue, wampende, wamtumikie Mungu na mwisho wote tupate kuiona mbingu.

UONGOZI

S/N

WADHIFA

JINA

KANDA

JUMUIYA

1

MWENYEKITI

LAURI TEMBA

MT. ANYESI

KRISTO MFALME

2

MAKAMU MWENYEKITI

DAMIANI DANIEL

MT. ANTON WA PADUA.

MT. KAROLI LWANGA

3

KATIBU

JANETH SHAYO

MT. PAULO MTUME

MT. RITHA WA KASHIA

4

KATIBU MSAIDIZI

TUMAINI CHIPA

MT. MAXIMILIAN KOLBE

MT. KATARINA WA SIENA

5

MWEKA HAZINA

DAUDI DEOKARI

MT. YOHANE MARIE VIANNEY

MT. FRANCIS XAVERY

 

Mt Rita ni Chama Cha Kitume cha Kumuenzi Mt Rita. Kwa Sala,Maombi na Novena Zake. Pia Ni Chama Kinachohusika na Kufanya Hija Manbalimbali ambazo Huwa zinafamyika Katika  Kituo cha Maria Rita Huko Mwanza. Pia Kufanya Matendo ya Huruma Kwa Wahitaji. Kilianzishwa Rasmi Tarehe 21 october 2023
Kwa Wanachama Kufanya Mafungo na Fr Mlezi wa Chama cha Mt Rita wa Jimbo la Dar es Salaam Fr Mgani. Na Wanachama 10 walipokelewa Rasmi katika Chama Hicho
Jumapili 22 October 2023 Katika Misa Takatifu Parokiani. Na Novena Zetu Kila Jumatatu ya Kwanza ya Kila Mwezi.

 

Tuliweka malengo ndani ya mwaka huu ambayo machache kati ya mengi tuliojiwekea tuliyafanikisha kama..

1.Darasa la malezi na makuzi ya kiroho.
2. Semina ya ndoa na familia ambayo bado inaendelea
3. Fellowship ya dekania kufanyikia kwetu..
4. Fellowship yetu ya kila juma pili

Malengo ni kuutafuta ufalme wa mungu kupitia karama au vipawa mbalimbali alivyotujalia mungu. Tuna malengo malengo ya kuendelea kuandaa semina mbalimbali kama

  1. semina ya vijana
  2. semina ya uwaka vile vile semina ya wawata..

Ni jumapili jioni saa kumi..Muda wa kukutana kwa ajili ya fellowship..(Sala zetu)Ni chama kitume au cha uamsho.

UONGOZI

S/N

WADHIFA

JINA

KANDA

SIMU

1

MWENYEKITI

DEOGRACE LUOGA

 

 

2

MAKAMU MWENYEKITI

STAPHORD KANYUNGU

MT. ANYESI

0657 - 461274

3

KATIBU

NICE JOSEPH

MT. ANYESI

0767 - 746445

4

KATIBU MSAIDIZI

ROSEMARY DIMOSO

MT. MAXIMILIAN KOLBE

0762 – 659886

5

MWEKA HAZINA

ANGELLAH AKILIMALI

MT. ANNE MARIE VIANNEY

 

Shirika la Wazee na Wastaafu la Mt. Augustino ni Chama cha Kitume kwa ajili ya wanaume na wanawake Wakatoliki Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea.

Hapa Tanzania lilianzishwa rasmi mwaka 1988 katika Parokia ya Kilema, Jimbo la Moshi. Katika Jimbo la Dar es Salaam utume ulianza mwaka 2003 katika Parokia 12 tu, sasa umeenea katika Parokia zaidi ya 145.

Katika Parokia ya Utatu Mtakatifu, Changanyikeni utume ulianza rasmi tarehe 12 Septemba, 2021 na hadi sasa kuna wanachama zaidi 128.

Majukumu ya Shirika la Wazee na Wastaafu Wakatoliki Tanzania (SWWWT)

Kwa mujibu wa Katiba la SWWWT, majukumu yake yameainishwa katika madhumuni tisa (9), ambayo ni:
1. Kuunganisha WWWT wa jinsi zote katika ngazi mbalimbali kuanzia Jumuiya Ndogo Ndogo za Katoliki(JNNK) hadi Taifa;
2. Kuwawezesha Wazee na Wastaafu kuishi maisha ya sala, ibada pamoja na kusoma na kutafakari neno la Mungu kwa lengo la kufikia utakatifu;
3. Wazee na Wastaafu wa Mt. Agustino watakuwa na siku ya moja ya sala kila wiki na Jumapili moja kila mwezi kulingana na utaratibu wa Shirika;
4. Kueneza habari njema miongoni mwa, katika shuke, JNNKna katika jamii nzima;
5. Kushauri na kusaoxi katika kukuza nidhamu na maadili ya wawtot, vijana na watu wazima katika nyanja mbalimbali;
6. Kuwawezesha Wazee na Wastaafu kuwa Saudi moja na hivyo watambuliwe na kanisa
7. Kubuni hali mbalimbali za kuwainua hali ya maisha ya wazee na wastaafu katika jamii:
8. Kuweka mipango na utaratibu wa kuhudumia washirika kama kundi wanapokabiliwa na matatizo; na
9. Kuwa na chombo cha kukuza na kudumisha uhusiano na ushirikiano wa wazee na wastaafu Wakatoliki katika mataifa mbalimbali.

Katika kutekeleza madhumuni hayo, katika Parokia ya Utatu Mtakatifu, wazee na wastaafu wanafanya yafuatayo:

(i) kila wiki siku ya Alhamisi saa 10 jioni wanachama wanapata fursa ya kusali na kulitafakari neno la Mungu kulingana na Mwongozo ulitolewa ni kutoka Agano la Kale na Agano Jipya;
(ii) kila Jumapili ya pili ya mwezi kuanzia saa 4.30 asubuhi baada ya misa ya pili wanachama hukutana kujadili masula mbalimbali kuhusu imani, kiuchumi na kijamii;
(iii) kufanya matendo ya huruma kwa kutembelea wagonjwa na wafiwa; na
(iv) kushirikiana na vyama vingine katika Parokia kuliimarisha Parokia yetu.

UONGOZI

S/N

WADHIFA

JINA

KANDA

SIMU

1

MWENYEKITI

RICHARD SILLO

MT. YOHANE MARIE VINNEY

0754 – 310443

2

MAKAMU MWENYEKITI

FORTUNATUS MKAWE

MT. PAULO MTUME

0715 – 584962

3

KATIBU

CATHERINE DANGATI

MT. VERONIKA

0786 – 731554

4

KATIBU MSAIDIZI

THERESIA BAYO

MT. ANYESI

0682 – 705406

5

MWEKA HAZINA

GEBRA MDUMA

MT. BERNADETHA

0715 - 338754